Mafunzo hayo yametolewa leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge yakiongozwa na wataalam toka vitengo na divisheni mbalimbali waliohudhuria mafunzo hayo ya mfumo mpya wa manunuzi katika ngazi ya mkoa.
Akitoa mada katika mafunzo hayo Kaimu mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi na Ugavi Bw. Revocatus Shaban amesema mfumo huu mpya wa NeST utasaidia kudhibiti rushwa na uwazi usioridhisha katika mchakato wa zabuni serikalini pamoja na kupunguza matumizi ya karatasi nyingi katika ujazajaji wa fomu mbalimbali wakati wa mchakato wa manunuzi(paper work).
Lakini pia mfumo huu mpya wa manunuzi ya umma kwa njia ya mtandao (NeST) utasadia kutatua changamoto zilizojitokeza katika mfumo wa zamani wa manunuzi wa TANePS,ambao ulianza kutumika mwezi Januari 1,2020.
Kuanzia tarehe 1 Oktoba manunuzi yote ya umma yatafanyika kupitia mfumo mpya wa NeST.NeST itasimamia usajili,zabuni,mikataba,malipo,katalogi pamoja na minada kwa njia ya mtandao.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa