Sikonge_Tabora
Watumishi wapya wa Idara ya Afya waliopangiwa kazi katika Vituo mbalimbali vya kutoa huduma za Afya Wilaya ya Sikonge wametakiwa kuzingatia sheria, na miongozo iliyowekwa na kufanya kazi kwa uadilifu.
Hayo yameelezwa katika kikao kilichofanyika Hospitali ya Wilaya ya Sikonge na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kutoa Elimu kwa watumishi hao.
Awali akifungua kikao hicho Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Dkt.Christopher Nyalu amewasisitiza watumishi hao kuwa waadilifu wakizingatia sheria na taratibu kwa za utendaji kazi huku wakiwaasa kuwa na Mahusiano mazuri mahali pa kazi.
Aidha, Dkt.Nyalu amewataka watoa huduma za Afya kuwa waaminifu katika ukusanyaji wa Mapato yatokanayo na utoaji wa huduma za Afya ili Serikali iweze kupata Mapato yatakayosaidia kuendeleza huduma kwa Wananchi.
"Kila Mtu humu ni Mkusanya mapato, Serikali inaingiza Mapato kupitia huduma zinazotolewa, hivyo ni vyema kuzingatia taratibu zilizowekwa za ukusanyaji wa Mapato"Dkt.Nyalu.
Kwa Upande wake Katibu wa Afya Hospitali ya Wilaya ya Sikonge Masoud Ally amewasisitiza kutoa huduma zilizo bora kwa wateja ili kuendelea kulinda sifa njema ya taasisi husika.
"Unapofanya jambo baya hautatajwa wewe Jina lako, ila taasisi unayofanyia kazi " Amefafanua zaidi
Sambamba na Hilo Mganga Mfawidhi wa Hospitali teule ya Wilaya ya Sikonge Dkt.Peter Songolo amewataka watumishi hao kutunza vyema Raslimali zilizo katika maeneo yao ya kazi .
Ofisi ya Mkurugenzi kupitia Idara Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe imetoa mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya wa Sekta ya Afya wakiwemo Madaktari na Wauguzi ambao wamepangiwa vituo vya kazi katika Hospitali na vituo vya Afya Wilaya ya Sikonge lengo ikiwa kuwajengea uwezo wawapo katika maeneo yao ya kitolea huduma.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa