Na.Anna Kapama_sikonge.
1.9.2022
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo amekutana na Kamati ya Afya ya Msingi Wilaya ya Sikonge ili kupanga Mikakati ya kufanikisha zoezi la Chanjo ya Polio kwa awamu ya tatu ambalo limeanza rasmi Leo.
Akizungumza wakati wa kikao na wajumbe wa Kamati ya Afya Msingi Wilaya ,DC Palingo amewapongeza wataalamu kwa kufanikisha vizuri awamu ya Pili ya zoezi la Chanjo ya Polio ambapo walichanja watoto 64,457 sawa na 128%.
Awali akisoma taarifa ya maandalizi na mwenendo wa zoezi Mratibu wa Chanjo Wilaya Muku Mbaga amesema Wilaya ya Sikonge imepokea dozi 71,000 na imelenga kutoa chanjo ya polio ya matone kwa watoto 66,769 wenye Umri chini ya miaka Mitano .
Kwa Upande wake Mganga Mkuu Wilaya ya Sikonge Christopher Nyalu amesisitiza timu zote kujipanga kikamilifu ili kufanikisha na zoezi hilo.
"Mazoezi kama haya tunategemea kwenye jamii tuweze kutoa ujumbe sahihi,na kujibu Maswali kwa wananchi Wanapouliza tujitahidi kuwapa ushirikiano" Dkt.Nyalu
Huduma ya chanjo ya Polio ya matone inatolewa katika Vituo vya kutolea huduma za Afya, nyumba kwa nyumba hivyo wananchi wanaombwa kutoa Ushirikiano kwa watoa huduma wanapopita katika nyumba zao.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa