Na Anastazia Maguha
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imeendesha zoezi la siku mbili la umezeshaji dawa kingatiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa Watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 14.
Akifungua zoezi hilo Kwa niaba ya Mkuu wa wilaya Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt.Christopher Nyalu amesema zoezi hili linajumuisha shule zote za msingi zilizopo Wilaya ya Sikonge ambapo watoto wote wenye umri wa kuanzia miaka 5 mpaka 14 waliopo nyumbani na shuleni watapatiwa dawa hizo.
"Watoto waliopo nyumbani watapitiwa na watendaji wa Afya watakao kuwa wanagawa dawa hizo naomba wazazi na walezi mtoe ushirikiano ili kwa pamoja tuweze kuwa na jamii yenye ustawi na afya bora"alisema Dkt.Nyalu
Aidha Dkt.Nyalu amesema lengo la serikali ni kuhakikisha jamii inakuwa yenye afya bora na ustawi na isiyodhoofishwa wala kunyanyapaliwa kwa kuwa na madhara ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele bali ni kuwa na jamii ambayo itachangia kikamilifu katika maendeleo binafsi na ya Taifa.
Kwa upande wake Kaimu Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele Jawed Zakaria alisema zoezi hilo la ugawaji dawa linafanyika katika zoni zote sita za wilaya ya Sikonge na wanategemea kumezesha watoto wasiopungua 64,320 elfu na kuwasihi Walimu kuhakikisha watoto wote wanapatiwa dawa hizo ili kuwawezesha kukua na kufanya vizuri darasani.
Ufunguzi huo umefanyika katika shule ya msingi Majengo iliyopo kata Sikonge yenye jumla ya Wanafunzi 1227.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa