WATENDAJI WA KATA WASISITIZWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA MADIWANI .
Sikonge_Tabora
Na.Anna Kapama
30.8.2022
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe.Rashid Magope amewasisitiza watendaji wa Kata kushirikiana katika kupeana taarifa mbalimbali hasa za miradi inayotekelezwa katika kila kata ili kujenga uelewa wa pamoja kwa Viongozi wa Kata wakiwemo madiwani.
Mhe.Mahope ametoa kauli hiyo Leo wakati akifunga Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Madiwani kwa robo ya Nne 2021/2022 katika Ukumbi wa Halmashauri na kuongeza kuwa miongoni mwa mambo yanayopaswa kuzingatiwa katika utendaji kazi wao ni kudumisha mawasiliano.
" Endeleeni kudumisha Mahusiano mazuri na Watendaji wa Vijiji, na Madiwani ..fedha zote za Maendeleo zinapokuja kwenye maeneo yenu lazima Madiwani wajue ..ni vizuri mkatimiza wajibu wenu kwa niaba ya Mkurugenzi, Mkifanya hivyo lazima mambo yaende vizuri" Mhe.Magope
Aidha, Mhe.Magope amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Seleman Pandawe pamoja na Watendaji wa Kata kwa kuendelea kusimamia miradi inayotekelezwa katika Wilaya hiyo sambamba Zoezi la Kitaifa la Sensa ya watu na Makazi.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa