Sikonge_Tabora
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo ameshuhudia utiaji Saini utekelezaji wa Mkataba wa Lishe uliofanyika kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge na watendaji wa Kata 20 za Wilaya hiyo.
Awali akizungumza na watendaji hao Mhe.Palingo amewataka kuzingatia na kutekeleza maelekezo yote yaliyo katika Mkataba huo ili kuwezesha kufikia lengo na jamii yenye Afya.
Aidha,amewaagiza watendaji wa Kata kuhakikisha wanasimamia shughuli za Lishe kwenye Shule zilizo katika maeneo yao ili Wanafunzi wapate Chakula wawapo Shuleni.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Nico Kayange amewataka watendaji kutoa taarifa sahihi za utekelezaji kila robo ambayo itakuwa unapima utekelezaji wa Mkataba huo.
"Tunataka tuwe na watu wenye Afya njema, tuepuke visingizio katika kutekeleza Mkataba na Afua za Lishe, taarifa za kila robo ziwe halisi". Kayange
Afisa Lishe Wilaya ya Sikonge Veronica Ferdinand amesema atahakikisha anafatilia utekelezaji wa Mkataba huo unatekelezwa kwa wananchi sambamba na kutoa Elimu ya Lishe ili kujenga jamii imara na yenye Afya.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa