Watendaji wa Kata na Waganga Wafawidhi katika Halmashauri ya Sikonge,wajengewa uwezo katika suala la ukusanyaji wa mapato kupitia mafunzo yaliyofanyika leo Tarehe 22.09.2023 katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sikonge yamelenga kuleta hamasa na uelewa wa kina juu ya suala nzima la ukusanyaji mapato ya Halmashauri.
Wawezeshaji wa mafunzo hayo wametoka katika idara na vitengo mbalimbali vya halmashauri ya Wilaya ya Sikonge,ikiwemo idara ya Fedha,Mazingira,Mipango,Tehama,Mapato,Biashara,Utamaduni,Kilimo na Mifungo pamoja na Idara ya Utumishi na Utawala.
Katika Mafunzo hayo wawezeshaji walijikita zaidi katika kuzungumzia Mifumo ya Ukusanyaji mapato inayofanyika kupitia POS, mfumo wa TAUSI pamoja na mifumo mingineyo.Vilevile wamesisitiza juu ya ukusanyaji mapato kwa kuzingatia upangaji wa bajeti,Uadilifu,kasi na kwa kuzingatia sheria za nchi.
Kwa upande wao Watendaji wa Kata na Waganga wafawidhi wameshukuru kwa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo katika ukusanyaji mapato na wameahidi kwenda kufanya kazi kwa bidii na kasi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa