Na, Edigar Nkilabo
Watendaji wa vituo wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), wanaoshiriki katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura wametoa tamko la kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kula kiapo cha kutunza siri katika majukumu yao, mbele ya Afisa Mwandikishaji wa Jimbo.
Zoezi hilo limejiri katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo Wananchi Sikonge FDC, ikiwa imesalia siku moja kuanza kwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura zoezi ambalo litaanza tarehe 1,Mei hadi tarehe 07 Mei,na kutoa fursa kwa wakazi wa Wilaya ya Sikonge kukagua taarifa zao za awali,kujiandikisha kwa wapiga kura wapya pamoja na kuhama vituo.
Aidha zoezi hilo ni mojawapo ya takwa la utekelezaji wa maadili na taratibu za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, zinazolenga kuhakikisha usimamizi wa uchaguzi unafanyika kwa haki bila upendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa