WATENDAJI na Viongozi mbalimbali kuanzia ngazi za vitongoji hadi Wilaya wametakiwa kuhakikisha wanasimamia sheria na kanuni zilizopo ili kukomesha utoro na mimba za utotoni mkoani Tabora
Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati wa kampeni zake za kutekeleza agizo la Waziri Mkuu alilolitoa wakati akizindua mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka huu na kuutaja Mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa utoro.
Alisema, haiwezekani aibu hiyo ikaendelea mkoani humo wakati upo mfumo wa serikali kuanzia ngazi ya kitongoji unaweza kusimamia jambo hilo la kulikomesha kwa kusimamia sheria na kanuni zilizopo ili kuwabana watoto watoro na wazazi wao.
Mwanri alisema kila mtu kuanzia mzazi, mwenyekiti wa kijiji, mtendaji kijiji, kata na Maafisa elimu kata wanatakiwa kusimamia majukumu yao kwa mujibu wa waraka wa elimu mwaka 2002 ili kukomesha utoro wa wanafunzi. Alisema hayo akihitimisha ziara yake katika Wilaya ya Sikonge ambapo alitembelea mradi wa ujenzi wa madarasa 5 na matundu ya vyoo 6 katika Shule ya Msingi Sikonge ambapo pia alipata furusa ya kutembelea darasa la pili na kujionea namna wanavyofundishwa stadi ya KKK na pia mradi wa ufugaji kuku ambao umepatiwa fedha na EQUIP-TZ kupitia mradi wao wa IGA.
Mthibiti ubora wa Shule Kanda ya Magharibi Kashindye Athumani aliwataka Maafisa Elimu Kata kutekeleza jukumu lao la kuthibiti ubora katika maeneo yao kwa kutembelea mara kwa mara katika shule zilizopo kwenye maeneo yao ikiwani kutaka kujua kama wanachofundishwa wanafunzi ni kile kilichoagizwa na pia kupambana utoro wa walimu na wanafunzi.
Alisema walimu wakuu nao wadhibiti utoro katika shule zao kwa kuangalia mahudhurio ya walimu na wanafunzi.
Aidha Kashindye aliwataka kuimarisha vitengo ushauri nasaha na nasihi ili kuwasaidia watoto kwa ajili ya kuepukana na utoro na mimba za utotoni shuleni kwao.
Alisema kuwa wasimamizi wa vitengo hivyo ni vema wakawa ni wale ambao wanaokubalika kwa wanafaunzi wengi ambao wanaweza kuwasikiliza na kukubalika sana kwa wanafunzi ili wanafunzi wawe na nafasi ya kupeleka na kueleza shida zao kwa uwazi bila kuogopa.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa