WATEKETEZA NYAVU HARAMU.
Jumla ya nyavu haramu 8 zateketezwa kwa moto katika Halmashauri ya wilaya ya Sikonge iliyopo mkoani Tabora.
Nyavu hizo ziliteketezwa na wataala wa sekta ya uvuvi kupitia Idara ya Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge baada ya kufanya Doria katika makambi ya uvuvi yaliyopo katika Mto Walla na bwawa la Igumila yote yanapatikana Sikonge na kubaini jumla ya nyavu 9 zilizokuwa zikitumika kuvua samaki walio chini ya kiwango kilichowekwa na mamlaka husika.
Wataalamu hao waliteketeza nyavu 8 kati ya nyavu 9 zilizokamatwa ambapo nyavu moja ilichukuliwa kama mfano wa kutolea elimu kwa jamii kuhepuka matumizi ya nyavu kama hizo kwani yanahatarisha raslmali za majini ikiwemo uvuvi wa vifaranga vya samaki.
Mtaalamu wa Uvuvi Bwana Evodius Wilbard akiteketeza nyavu haramu zilizokamatwa wakati wa doria.
Doria hiyo ililenga kutokomeza uvuvi haramu kwa kukagua wote waliopewa vipali kama wanavua kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu ambazo ziliwekwa kaatika kibali ambacho walikabidhiwa wavuvi hao.
Akitolea ufafanuzi Afisa Uvuvu wa Halmashauri ya Sikonge Bwana Evadius Wilbard alisema lengo la doria lilikuwa ni kuhamasisha wananchi kukata leseni Halali za uvuvi ili wapate sifa ya kuvua kwenye mabwawa na mito ambayo yameruhusiwa.
Ikumbukwe mwishoni mwa mwezi wa kwanza mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Peter Nzalalila aliagiza wataalamu kwenda kuhamasisha wananchi juu ya uvuvi na namna ya kupata leseni kwani kumekuwa na malalamiko ya baadhi ya wanachi walioko maeneo yanayozunguka bwawa hulo kuhusu wao kunyimwa vibali vya kuvua katika mabwawa hayo na vibali hivyo kupewa watu wanaotoka maeneo mengine.
Bwana Wilbard alifafanua kuwa elimu kwa wananchi inaendelea kutolewa kwani wengi wao bado wana dhana ya kuwa wao ni wazawa wa eneo husika hivyo hawaoni umuhimu wa kupewa leseni lakini kutokana na uhamasishaji unaoendelea wananchi wamekubali kuyapokea mabadiliko hayo na wamehaidi kutoa ushirikiano ikiwa ni pamboja na kukata kibali.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa