Na.Anna Kapama
Wataalamu kutoka Bodi ya Bonde la Ziwa Tanganyika wamefika Wilaya ya Sikonge Kata ya Ngoywa katika Kidakio Cha Mto Ulua kukagua na kutazama mienendo ya njia za Maji ya Mto huo.
Katika ukaguzi huo wataalamu hao wamewaasaa Wananchi hasa wafugaji na wakulima kutoendesha shughuli za binadamu katika vyavzo hivyo na badala yake ikiwa wanataka kutumia Maji ya Mto huo wafuate taratibu sahihi ili kutoathiri mkondo huo wa Mto.
Akizungumza na Viongozi wa Kijiji hicho Afisa kutoka Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Tanganyika Mhandisi Gaudens Ndolo amesema wananchi wanapaswa kufata taratibu na sheria za utunzaji wa Vyanzo vya Maji zilizowekwa.
"Wananchi wanaruhusiwa kuendesha shughuli zao umbali wa Mita 60 kutoka kwenye Chanzo Cha Maji, sasa kuna watu waliojenga matuta wakichepusha Maji, kwa kufanya hivyo wanauzuia Mto kuendelea ,niwashauri waombe kibali kutoka mamlaka husika wataelekezwa namna Bora ya kutumia pasipo kuathiri Mto huo" Mhandisi Ndolo
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kijiji Cha utimule Charles Edward amesema Uongozi wa Kijiji utahakikisha wananchi wanapata Elimu ya kutosha ili waweze kutunza Kidakio hicho.
"Nawashukuru wataalamu kwa kuja kutupa Elimu hii,,sisi Viongozi tutasimamia, na watakaokaidi tutawawajibisha" Bw.Charles Edward amefafanua.
Kidakio Cha Mto Ulua kimekuwa na tija kwa wananchi wa Kata ya Ngoywa na maeneo mengine katika Shughuli za Kilimo na Ufugaji hali inayopelekea wataalamu wa Bonde la Ziwa Tanganyika kufika kutoa Elimu ya utunzaji wa chanzo hicho ili kidumu kwa muda mrefu.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa