WATAALAMU KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WATEMBELEA HOSPITALI YA WILAYA.
SIKONGE_
27 Juni, 2022
Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango imefika Wilaya ya Sikonge kufuatilia na kufanya tathmini ya Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kupitia athari za Kijamii na Kiuchumi zitokanazo na UVIKO-19 .
Timu hiyo imefuatilia majengo mawili ya Afya Katika Hospitali ya Wilaya ya Sikonge ambayo ni Jengo la Kuwahudumia Wagonjwa wa dharula (EMD) lenye thamani ya TSH.Milioni 300, pamoja na Nyumba ya Mtumishi ambayo imegharimu Tsh.Milioni 90.
Aidha, Wataalamu hao wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji Seleman Pandawe kwa kusimamia vyema Miradi hiyo ambapo Jengo la EMD limefikia Asilimia 93% huku Nyumba ya Mtumishi ikiwa imekamilika kwa asilimia 100%.
Na.Anna Kapama
#jiandaekihesabiwa
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa