PPRA YAENDESHA MAFUNZO YA MFUMO WA UNUNUZI WA UMMA (NeST) KWA WADAU MBALIMBALI WILAYANI SIKONGE.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Seleman Pandawe amepokea timu ya wataalam toka Mamlaka ya Udhibiti wa ununuzi wa umma kanda ya kati na magharibi waliofika kuendesha mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa umma kwa wadau mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Akieleza dhima nzima ya mafunzo hayo Kaimu Meneja wa PPRA kanda ya kati na magharibi Bi. Suma Atupele amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwafikia wadau moja kwa moja na kutatua changamoto zao wanazokutana nazo wanapokuwa wakitumia mfumo wa ununuzi wa umma (NeST).
Ametoa wito kwa wajasiriamali wadogo wadogo wasiogope kutumia fursa zinazotokana na mfumo huu mpya wa ununuzi wa umma kwa kigezo cha kuwa na mitaji midogo na amesisitiza maafisa biashara kuendelea kuwasaidia wafanya biashara hao kujisajili kwa wingi.
Vilevile amesisitiza wadau kufanya makisio halisi kwa kuzingatia jiografia ya eneo husika ambapo mradi unatekelezwa. “Thamani halisi ya kile kinachojengwa lazima ionekane,gharama za miradi ziende sambamba na gharama za usimamizi wa miradi hiyo,huwezi kuwa na mradi usio na gharama za usimamizi.amesema Bi. Atupele.
Mafunzo hayo yamegusa makundi mbalimbali ya wadau wa mfumo wa ununuzi wa umma wakiwemo,Waganga wafawidhi,Walimu wakuu,Wakuu wa shule,Watendaji wa Kata,Wakuu wa Divisheni na Vitengo,Wazabuni pamoja na mafundi ujenzi.
Mwisho amewapongeza sana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa kufanya uratibu mzuri wa zoezi la mafunzo haya kuweza kufanyika kwa muda mfupi wa maandalizi, lakini pia amempongeza Mbunge wa jimbo la Sikonge Mhe. Joseph George Kakunda kwa hoja yake aliyoiwasilisha PPRA kuwatetea mafundi ujenzi (local fundi) wa Sikonge nao waweze kupatiwa elimu ya mfumo mpya wa ununuzi wa umma ,kwani hapo awali mafundi hawa walipokuwa wakiingia katika mfumo huu walikuwa wanashindwa kuona kazi wanazotaka kuziomba .
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa