Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe ameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata na vijiji. Lengo la mafunzo haya ni kuhakikisha kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa unatekelezwa kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa.
Akifungua mafunzo hayo, msimamizi wa uchaguzi amesisitiza washiriki umuhimu wa kufuata sheria, kanuni, na taratibu ili kuepuka matendo yanayoweza kuleta taharuki. "Ni muhimu kufuata falsafa ya 4R ya Rais Samia Suluhu Hassan ili zoezi hili liweze kufanyika bila mivutano isiyokuwa ya lazima,"ameeleza Ndg. Pandawe.
Wakisisitiza umuhimu wa kuimarisha maadili ya uchaguzi. Wawezeshaji wamekumbusha washiriki kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili na kuepuka vishawishi vyovyote vinavyoweza kusababisha ubaguzi au vurugu wakati wa uchaguzi.
Naye Afisa Uchaguzi wa Wilaya, Ndg. Geofrey Mwilawa, amewaelekeza wasimamizi wasaidizi kuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa sahihi kuhusu uchaguzi, na kuwakumbusha kupinga taarifa zinazoweza kupotosha ukweli wa uchaguzi huo.
Mafunzo hayo yameambatana na kiapo cha uadilifu kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kilichotolewa na Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya mwanzo Mhe. Kasian Amando Nyami.
Mafunzo haya ni hatua muhimu katika kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa unafanyika kwa ufanisi na kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa, huku ikilenga kuimarisha demokrasia na ushirikiano katika jamii.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa