Wapatiwa mafunzo.
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora wapatiwa mafunzo ya mfumo wa mipango na bajeti wa mamlaka ya serikali za mitaa wa PLANREP na mfumo wa uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha kwenye vituo vya kutolea huduma FFARS.
Mafunzo yalitolewa kwa muda wa siku mbili na wataalam wa ndani Halmashauri ambao pia walipatiwa mafunzo mkoani na wataalam kutoka OR-TAMISEMI walikuwa na jukumu la kutoa mafunzo kwa watumiaji waliopo katika idara na vitengo vingine kwenye Halmashauri.
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Sikonge wakimsikiliza kwa makini muwezeshaji.
Mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha watumiaji kufanya shuguli zao kwa urahisi. Pia kulikuwa na mabadiliko yaliyofanya kwenye mfumo ili kusaidia kuondoa muingiliano wa baadhi ya fedha kupelekwa kwenye idala isiyokusudiwa.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa