WANUSURIKA KIFO
Abiria kadhaa waliokuwa safarini kutokea Mpanda kuelekea Arusha wanusurika kufa baada ya gari walilokuwa wanasafiria kuacha njia na kupinduka
Gari hilo lenye namba T619 kampuni ya Coast Line lilipata ajali eneo la Koga kata ya Ipole wilayani Sikonge Mkoani Tabora amapo kwa kawaida hufanya safari zake kati ya Mpanda na Arusha.
Akizungumzia namna tukio lilivyotokea mmoja wa maafisa wa usalama barabarani ambaye pia alikuwa eneo la tukio alisema kuwa majira ya saa nne asubuhi kulitokea ajari maeneo hayo huku akimtaja dereva aliyefahamika kwa jina la Adam Titi kuwa aliendesha upande usio sahii kwake ambapo alikutana na janksheni iliyopelekea gari hilo kukosa muelekeo na hatimaye kupinduka. Afisa huyo alitaja chanzo kuwa ni uzembe wa dereva ndio uliopelekea kutokea kwa tukio hilo.
Naye muuguzi Muhudumu wa Hospitali ya Misheni Bi. Veronica Zakaria alithibitisha kupokea majeruhi wawili ambao ni Amina Yohana (40) pamoja na Leticia Christian (23) walio pata mshituko wakati wa ajari na kusema kuwa waliwapatia huduma ya kwanza na hali zao zilikuwa zinaendelea vizuri.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Sikonge akipokea Maelezo ya mmoja wa Majeruhi aliyelazwa katika Hospitali ya Misheni
Akisimulia alivyoweza kunusulika Bi Amina alipongeza sheria za usalama barabarani zinazowataka abiria wote kufunga mkanda wawapo safarini kwani jambo hilo limeweza kumuokoa yeye kupata majeraha makubwa zaidi kwani alikuwa amefunga mkanda.
Akitoa pole kwa niaba ya mkuu wa wilaya, katibu tawala wa Wilaya ya Sikonge Renatus Mahimbali. Aliwaasa madereva wote kufata kanuni na taratibu za barabarani kwa wanakuwa wamebeba maisha ya watu sanjari na hayo pia wanatakiwa kuwalinda hata watumiaji wa barabara kwani uzembe unahepukika
Kuntu ya hayo Mahimbali Pia alifika eneo la tukio ili kujionea hali halisi ya nammna ajali ilivyotokea pamboja na kuwatembelea majeruhi walio lazwa katika kituo cha afya Misheni ili kuwajulia hali na kuangalia namna watakavyowasaidia baada ya kupatiwa matibabu waendelee na safari zao.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa