Na Linah Rwambali
Maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya Wanawake kwa mkoa wa Tabora yamefanyika katika Halmashauri ya Nzega Mji katika uwanja wa Samora ambapo maelfu ya wanawake walihudhuria katika sherehe hiyo.
Akihutubia hadhara iliyohudhuria maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mkuu wa Wilaya ya Urambo Dkt.Khamisi Mkanachi alisema wanawake wana nguvu ya pekee ambayo ikitumika ipasavyo inaweza kuchangia maendeleo katika taifa letu.
Aidha, Dkt.Mkanachi aliwakumbusha wanawake kuzingatia suala la malezi ili kujenga kizazi bora.
"Ndugu zangu kwa sasa kuna changamoto ya mmonyoko wa maadili hivyo niwaombe wanawake wote, pamoja na kuwa na majukumu ya utafutaji msisahau kuhusu malezi. Mtenge muda wa kuzungumza na kusikiliza watoto wenu" alisema.
Mbali na hayo Mkanachi aliwahimiza wanawake waliohudhuria katika sherehe hiyo kuachana na matumizi ya mkaa na kutumia nishati Safi.
"Ninawakumbusha matumizi ya nishati Sababu ni rahisi na salama kutumia" alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe.Naitapwaki Tukai aliwaasa wanawake kushikamana na kupendana ili kuleta maendeleo miongoni mwao.
“Tushikamane na kubebeana mizigo ukiona mwenzio anachangamoto fulani ibebe kama yako ili woe tuwe na maisha mazuri”alisema.
Kaulimbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake ni Wanawake na Wasichana 2025, Tuimarishe Haki,Usawa na Uwezeshaji”.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa