WANAWAKE NA UONGOZI
Wanawake waaswa kugombea nafasi Mbali mbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa unaotegemewa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2019.
Kauli ambayo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri kwenye maazimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kiwilaya yalifanyikia kata ya Misheni Wilayani Sikonge.
Siku hiyo ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka na kwa mwaka huu ikiwa imebeba kauli mbiu ya “Badili Fikra kuelekea Usawa wa Kijinsia na Maendeleo Endelevu’’
Mhe. Magiri alisisitiza wanawake kujitokeza kuwania nafasi mbali mbali zitakapotangazwa ili kuwawezesha kufikia usawa wa kijinsia kama wanavyoudai katika kauli mbiu yao ya mwaka huu.
Akitolea mifano ya wanawake mbali mbali ambao wamepata nafasi za juu katika serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. John Pombe Magufuri. Mkuu wa wilaya amewataja Mama samia, Ummy Mwalimu na Dkt. Tulia kama wanawake wanaofanya vizuri baada ya kuaminiwa na kupewa uongozi.
Wanawake wa Wilaya ya Sikonge wakiwa katika Maandamano
Hivyo basi ni wito wake kuwaona wanawake wa Wilaya ya Sikonge wakifika mbali zaidi kwani hata kwenye Baraza la Madiwani Wilayani hapa kumekuwa na idadi kubwa ya wawakilishi wanawake jambo ambalo ni kielelezo tosha cha namna mama anavyoweza.
Katika sherehe hiyo iliyopambwa na vikundi mbalimbali vya Burudani ilianza kwa maandamano kutokea Barabara ya Migundini mpaka viwanja vya misheni ambapo baadae kwaya maalumu iliimbwa ikipongeza jitihada za wanawake na kukumbushia mazuri yote yaliyofanywa na wanawake waliopewa nafasi.
Shule ya Sekondari kamagi nao hawakubaki nyuma kwa kutoa igizo la jinsi ya kumsaidia mtoto wa kike apate elimu.
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Sikonge inaongozwa na Mkurugenzi Mwanamke ambaye ni Bi. Martha Luleka wakati huohuo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sikonge naye ni Mwanamke Bi. Anna Chambala, kuntu ya hayo idadi kubwa ya Madiwani wanawake jimbo hili limekuwa jambo la kujivunia wanawake waishio wilaya hii kwani wametendewa haki hata kwenye uongozi ukiachilia mbali watumishi wanawake waliopo katika idara nyingine za kiutumishi.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa