WATEMBEA KM 9 KUFATA ELIMU.
WANAFUNZI wanaokaa kijiji cha Ulilwansimba kilichoko kata ya Misheni Wilayani Sikonge mkoani Tabora, wanalazimika kutembea Km 9 kufuata elimu.
Wanafunzi hao wa elimu ya msingi hutembea kuelekea Shule ya YombaKulovya iliyopo umbali wa Km. 4.5 kutoka kitongoji cha Ulilwansimba jambo linalopelekea kiwango cha ufauru kushuka kutokana na umbali huo ukilinganisha na umri mdogo wa wanafunzi hao kuweza kumudu masomo na mwqendo kwa wakati mmoja.
Akizungumzia jitihada za Serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo Diwani wa kata ya Misheni Mhe. Juma Ikombola alisema kuwa wamepokea jumla ya shilingi Ml 156.6 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa, matundu sita ya vyoo pamoja na nyumba moja ya walimu ijulikanayo kama two in one.
Mh. Ikombola aliongeza kuwa mbali na hayo wanakijiji wa Ulilwansimba pia walishaanza jitihada mapema kwa kujenga shule shikizo ambayo ina madara mawili ambayo ni darasa la awali pamoja na darasa la kwanza na tayari limesajili wanafunzi wa mwaka huu hivyo basi ukamilishwaji wa madarasa yanayofuatia utawaokoa wanafunzi wengi kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta eleimu.
Sanjari na hilo wanakijiji pia walijitokea kusafisha eneo na kuchimba msingiikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu. Akisisitiza umuhimu wa kujitolea Bi. Clementina Kadiko ambaye ni mtendaji wa kijiji cha Usupilo alisema kuwa wamejipanga kutumia nguvu ya wananchi pamoja na pesa iliyotolea na Serikali ili kupata ongezeko la Ofisi ya walimu pamoja na vyumba vingine vitatu vya madarasa kwani matofali tayari yapo.
Diwani wa kata ya Misheni Mhe. juma akishirikiana na wananchi kusafisha eneo litakalojengwa Shule ya Msingi Ulilwansimba
Akizumgumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Bi. Faraja alisema kuwa shule ni mali ya kijiji husika hivyo kuwaasa wanakitongoji wa Ulilwansimba kujitolea kwa moyo wote kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa shule hiyo kwa ubora na muda waliopangiwa. Vilevile alitolea mfano swala la wanafunzi kushindwa kwenda shuleni kipindi cha masika kutokana na mito kujaa maji. Bi Faraja alisema kuwa linahepukika iwapo shule itakamilika.
Akitoa shukrani za dhati kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi mwenyekiti wa CCM Kata ya Misheni alisema kuwa ni jitihada za Serikali kuhakikisha wananchi wake wanaboreshewa miundombinu ikiwemo ya Elimu hivyo basi kilichofanyika ni kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa