WANANCHI SIKONGE WAENDELEA KUJITOKEZA KUPATA CHANJO YA UVIKO-19.
Wananchi kata ya Kipili wamejitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo alipotembelea kata hiyo akiambatana na watoa huduma za Afya akiwemo Kaimu Mganga Mkuu(W).
Akizungumza na wanachi hao katika Mkutano wa hadhara,Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo amewahamasisha wananchi kata ya Kipili kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 kwa kuchanja kwa hiari kwani ni muhimu na kuongeza kuwa Serikali ina nia njema ya kulinda taifa lake.Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuwapuuza baadhi wa watu wenye nia ovu wanaopotosha kuwa chanjo si salama.
"Chanjo ni salama,ni hiari na ni muhimu"DC Palingo aliongeza.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu (W)Dr.Theopister Elisa ametoa elimu juu ya faida anazopata mtu aliyepata Chanjo ya UVIKO-19 ikiwa ni pamoja na kuongeza kinga ya mwili dhidi ya ugonjwa huo,inapunguza uwezekano wa mtu kupoteza maisha endapo atapata ungonjwa huo.
Aidha,Dr.Elisa amesema dozi za chanjo zimesambazwa katika vituo vyote vya afya,zahanati zilizopo Wilayani hapo na kuwasisitiza wananchi waendelee wajitokeza kupata huduma hiyo kwa hiari ili kujikinga dhidi ya UVIKO-19.
Na.Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa