• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Sikonge District Council
Sikonge District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Idadi ya Watu
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Mifugo na uvuvi
      • Afya na Ustawi wa jamii
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mazingira na Taka ngumu
      • Kilimo, Umwagilaji na Ushirika
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Uchimbaji wa Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo Ndogo
    • Miongozo Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya sanaa
      • Sanaa za picha
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba
    • Habari mpya
    • Matukio

WANANCHI JITOKEZENI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Imewekwa: July 1st, 2019

WANANCHI JITOKEZENI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI   LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.

SIKONGE Wananchi wahimizwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mara muda utakapotimia.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya  Sikonge Mhe. Peter Nzalalila alipokuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za maadhimisho ya Serikali za Mitaa Wilayani hapa yaliyofanyika katika Kata ya Mkolye na kuhuzuliwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya pamoja na wataalamu wa Halmashauri.

Katika serehe hizo Mhe. Nzalalila alisema kuwa hivi sasa serikali inaelekea katika uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji hivyo basi ni vyema jamii ikajiandaa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo muhimu.

“serikali inaanzia ngazi za vitongoji kwenda mpaka juu tunapompata Waziri mwenye dhamana ambaye ni Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)” alifafanua ili kuwapa picha halisi ya namna uchaguzi huo ulivyo muhimu.

Aidha alitoa hamasa kwa wananchi kujiandaa na uchaguzi huo kwa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi zitakazosaidia uboreshwaji wa daftari hilo.

Umati wa Wananchi wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi Mhe.Nzalalila (hayupo pichani) siku ya maazimisho ya Serikali za Mitaa Mkolye.

“wakati utakapofika wote tujitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili tupate haki yetu ya msingi ambayo ni kumchagua kiongozi bora anayefaa kutuongoza kwa miaka mitano ijayo” alisema.

Awali Diwani wa kata ya Mkolye Mhe. Seif Mayoka alisema kuwa hali ya kisiasa katika kata hiyo ni nzuri na wananchi wana imani kubwa kwa Serikali ya  Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na kutekeleza vyema ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 kama ilivyoahidi. Aliongeza kuwa wana Mkorye hawataiangusha serikali yao katika uchaguzi ujao wa serikali za Mitaa ambao utafanyika nchi nzima.

Maadhimisho ya Serikali za mitaa hufanyika kila tarehe moja ya Mwezi wa Saba ambapo Wilayani Sikonge huadhimisha sherehe hizi kwa burudani mbalimbali na wananchi hupata fursa ya kusikiliza kutoka kwa viongozi mbali mbali namna serikali inavyotekeleza kwa upande wa Serikali za Mitaa.


TEHAMA SIKONGE

Matangazo

  • TANGAZO LA ZABUNI YA KUKODISHA CANTEEN [MGAHAWA] MPYA KWENYE JENGO LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZAABUNI YA KUMPATA MWEKEZAJI KATIKA KIWANDA CHA KATI CHA KUCHAKATA MAZAO YA NYUKI(MARUDIO) June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA USAFI KWENYE OFISI ZA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA ULINZI June 07, 2023
  • Angalia zaidi

Habari Mpya

  • MJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA WILAYANI SIKONGE

    May 07, 2025
  • KIKAO CHA TATHIMINI YA MKATABA WA LISHE WILAYANI SIKONGE

    April 29, 2025
  • WATENDAJI WA INEC WILAYANI SIKONGE WAMEKULA KIAPO CHA UADILIFU, KUJIWEKA KANDO NA VYAMA VYA SIASA.

    April 29, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE YAADHIMISHA MIAKA 61 YA MUUNGANO KWA KUFANYA USAFI

    April 26, 2025
  • Angalia zaidi

Video

Ziara ya Waheshimiwa Madiwani Wilayani Rungwe - Mbeya.
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Zabuni
  • Matukio
  • Matangazo
  • Habari

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Mkoa wa Tabora
  • TAMISEMI
  • Urambo DC
  • UTUMISHI
  • Kaliua DC

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC

    Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora

    Simu: 0767135460

    Simu: 0767135460

    Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma zetu

Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa