Sikonge_Tabora
Na.Anna Kapama
Wakati zoezi la usajili wa wakulima kwa ajili ya kupata mbolea ya ruzuku ya Serikali likiendelea Afisa Kilimo na Ushirika Wilaya ya Sikonge Hashim Kazoka anaendelea kuwasisitiza wakulima Wilayani hapo kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha na kusajiliwa kwenye Mfumo wa ruzuku ya Serikali katika Ofisi za Vijiji bure.
"Mkulima akijiandikisha kwenye Ofisi ya Kijiji akasajiliwa anaweza kupata mbolea kwa bei ya Tsh 60,000/= hadi Tsh.70,000/= badala ya Tsh.120,000 hadi Tsh.140,000 kwa mfuko mmoja Wa kilo 50 kwa mawakala wa Usambazaji wa mbolea watakaokuwa wamewekwa, hivyo wakulima waendelee kujiandikisha kwa kuwa zoezi bado linaendelea " Kazoka
Aidha, Bw.Kazoka ameongeza kuwa mpaka sasa wakulima zaidi ya 13,000 Wilaya ya Sikonge wamejiandikisha na kusajiliwa kwenye Mfumo kwa Msimu wa Kilimo 2022/2023.
Kwa Upande wao baadhi ya wakulima wameishukuru Serikali kwa kuwashika Mkono wakulima ambao wanatarajia kujikwamua kiuchumi kupitia Kilimo ambapo awali walishindwa kumudu gharama za Kilimo kutokana na kupanda kwa bei ya Mbolea hivyo kupelekea wengi wao kutojihusisha shughuli za Uzalishaji kupitia kilimo.
"Kwa kweli naishukuru Serikali ya mama Samia ,kupitia kushuka kwa bei ya mbolea nategemea kulima na kujikwamua kiuchumi tofauti na mwaka jana ambao sikulima kabisa" Mkazi wa Kijiji Cha tulieni_sikonge
Katika mwaka wa fedha wa 2022/2023, Serikali imepanga kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima nchini. Mpango unaolenga kupunguza gharama ya mbolea kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo na kuimarisha usalama wa chakula. Ruzuku itatolewa kwa wakulima waliosajiliwa kupitia daftari maalum ngazi ya Kijiji na kuingizwa kwenye mfumo wa kieletroniki.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa