WAJASILIAMALI WAPIGWA SEMINA.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Agrey Mwanri azungumza na wajasiliamali Wilayani Sikonge na kuwataka kuchukua vitambulisho ili kuepukana na bugdha za kulipa kodi.
Katika semina yake Mhe. Mwanri alitoa elimu juu ya makundi yanayohitaji kulipa kodi ikiwemo washona viatu, waganga wa kienyeji n.k. akisisitizia swala hilo pia alisema kuwa yeyote asiyetaka kubadilika tutambadilisha ili aendane na kasi yenye maendeleo.Aliongeza kuwa kiongozi yeyote anayeenda kuwashawishi wananchi kuhusu kutochukua vitambulisho anapaswa kupuuzwa kwani haitakii mema nchi ya Tanzania.
Sanjari na hayo viongozi wengine walioambatana na mkuu wa Mkoa alikuwepo pia Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Peter Nzalalila ambaye aliahidi kufatilia kwa ukaribu ili kubaini matatizo yanayokwamisha vitambulisho kwa wakati uliopangwa na kubaini namna ya kuzitatua.
Mkuu wa Mkoa akizungumza na wajasiliamali wilayani Sikonge
Pia aliwaasa watendaji kuwa na mpango kazi pamoja na mkakati katika kutekeleza majukumu yao hivyo kuhakikisha vitambulisho vinaisha ndani ya wiki moja kama walivyopewa.
Wananchi zaidi ya 50 walijitokeza kuorodhesha majina yao ikiwa ni ahadi ya kuchukua vitambulisho ndani ya wiki moja idadi hii ikiwa ni jumla ya kata nne alizotembelea mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuhamasishaambazo ni Ipole, Sikonge, Tutuo na Pangale.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa