Wajasiliamali tabora waula.
Mkoa wa tabora wazindua rasmi vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga. Ikiwa ni kutekeleza agizo la Mhe. Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Uzinduzi huo ulihuzuliwa na wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wenyeviti wa Halimashauri naviongozi wa ulinzi na wafanyabiashara, vilevile kulikuwa na maandamano ya wafanyabiashara ambao waliomba kuandamana ili kumpongeza Dkt. Magufuli kwa kuuthamini na kuutambua mchango wao katika sekta ya uchumi wa viwanda.
Mkuu wa wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magili akiandamana na wafanyabiashara
Akizindua vitambulisho hivyo mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Agrey Mwanri alisema kuwa mkoa wa Tabora ulipokea jumla ya vitambulisho elfu ishirini na tano (25,000) na kila wilaya imekabidhiwa vitambulisho 3125, ambapo alisisitiza kuwa vitambulisho hivyo vitatolewa bure kwa wafanyabiashara wenye mtaji chini ya shilingi milioni nne kwa mwaka ila mfanyabiashara atachangia shilingi elfu ishirini tu.
Mwanri alisema ‘’jitihada za raisi ni kuinua wanyonge ili kuelekea uchumi wa viwanda hivyo ni razima tuwashike mkono wafanyabiashara hawa wadogo, tukiwaacha watatumbukia shimoni” aliongeza kuwa “ ni marufuku kwa machinga yeyote kusumbuliwa katika biashara yake, mama ntilie kumwagiwa vyakula vyao iwe mwiko”
Mbali na hayo mkuu wa mkoa pia alisisitiza majosho na ranchi zote zilizopo katika Halimashauri za mkoa Tabora zifufuliwe. Pia kila wilaya itapatiwa matrekta ili kurahisisha kilimo cha kisasa. “ ni marufuku kilimo cha ovyo ovyo katika mkoa wa Tabora” Pia aliusifia mkoa wa sikonge kwa uzalishaji wa asali na Tumbaku.
Mkurugenzi mtendaji wa Halimashauri ya wilaya ya Sikonge Mhe. Martha Luleka akifurahia jambo wakati wa uzinduzi.
Akipokea vitambulisho mkuu wa wilaya ya Sikonge Ndg. Pelesi aliwasisitiza wafanyabiasha kuvitunza vizuri vitambulisho hivyo na kusema kuwa vitatolewa kwa haki. Wanaostahili kupewa wote watapewa.
Wafanya biashara pia waliahidi kuzingatia miongozo yote iliyotolewa na kutunza kutunza vitambulisho. Waliiomba serikali kuwatengea maeneo mahalumu ya kufanyia biashara pia kuongeza vitambulisho hivyo hadi kijijini na kuziomba taasisi za kifedha kuvitumia kuwapatia mikopo.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa