Na, Anastazia Maguha
Wananchi zaidi ya 400 wilayani Sikonge wamenufaika kwa matibabu mbalimbali ya kibingwa kupitia programu ya Madaktari Bingwa wa Rais Dkt.Samia, ambapo kambi ya Madaktari Bingwa wa aina sita na Muuguzi mbobezi wa chumba cha upasuaji imetoa huduma kwa wananchi hao kwa muda wa siku tano.
Daktari Bingwa wa Watoto na kiongozi wa timu ya Madaktari hao Dkt.Lyimo Michael amesema zoezi la utoaji wa matibabu limefanikiwa kwakiasi kikubwa kwakuwa wananchi wengi wamehamasika na kujitokeza kwa wingi katika Hospitali ya Wilaya na kupatiwa matibabu stahiki.
“Ndani ya hizi siku tano tumefanikiwa kuona wagonjwa zaidi ya 400, robo tatu ni wagonjwa wan je wapatao 250 na 150 ni wagonjwa waliolazwa”alisema Dkt.Lyimo.
“Magonjwa yanayoongoza kwa Watoto ni selimundu(sickle cell) na malaria kali inayosababisha kuharibika kwa figo pamoja na maambukizi ya bakteria kwa watoto wachanga na kwaupande wa upasuaji wananwake wanachangamoto ya vimbe kwenye via vya uzazi(Ovarian cisty) na Henia kwa wanaume”aliongeza.
Aidha Dkt.Lyimo amesema magonjwa ya ndani yaliyoonekana kuongoza ni presha,vidonda vya tumbo na homa yabisi ambapo wataalamu wamehakikisha wanawahudumia wagonjwa wote waliopatikana na changamoto ya magonjwa hayo.
Naye Mocha Shimba ambaye ni mkazi wa kata ya Mpombwe ameushukuru uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Sikonge na Rais Dkt.Samia kwa kusogeza huduma za matibabu ya kibingwa kwani wananchi wengi wamenufaika nan huduma hizo kwa gharama nafuu.
“Nimefika hapa na mwanangu anaumwa nimepokelewa vizuri amefanyiwa matibabu na kupatiwa dawa kwa gharama ndogo tofauti na kufuata huduma hizo kwenye hospitali za rufaa”alisema.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Sikonge Dkt.Catherine Katisho amesema huduma hizo za kibingwa zimeenda sambamba na kuwajengea uwezo wataalamu wa afya wa Hospitali ya Wilaya.
“Wananchi wetu wamepata huduma lakini nitoe wito kwa wananchi kujitokeza tangu siku ya kwanza ili kupata huduma kwa wakati na kunufaika na huduma hizi za kibingwa kwa gharama nafuu”Dkt.Katisho.
Matibabu hayo ya kib ingwa yalianza kutolewa tarehe 29/09/2025 na kufikia tamati tarehe 03/10/2025.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa