WAFUGAJI WATAKIWA KUEPUKA KUCHUNGIA MAENEO YA HIFADHI.
Mkurugenzi Mtendaji(W) Selemani Pandawe amewataka wafugaji katika Hifadhi ya msitu wa asili Nyahua kufuata sheria na taratibu za ufugaji hasa maeneo yaliyo karibu na hifadhi ikiwemo kutoingiza mifugo hifadhini kwa ajili ya malisho ili kujiepusha na faini wanazotozwa baada ya kukamatwa.
Mkurugenzi ameyasema hayo alipokutana na viongozi wa wafugaji,maafisa maliasili pamoja na baadhi ya wafugaji kufuatia mgogoro uliokuwepo kati Maafisa maliasili na wafugaji waliokamatwa katika hifadhi hiyo.
Aidha,DED Pandawe ametumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wa wafugaji wasisubiri kutatua migogoro inapowafikia ofisini bali watoe Elimu kwa wafugaji juu ya sheria mbalimbali ambazo imebainika wafugaji wengi hawazifahamu ili kuepuka matatizo yanayojitokeza.
“viongozi fanyeni majukumu yenu..tengenezeni majukwaa ya kuwaelimisha na ikibidi waiteni wakuu wa Idara husika watoe Elimu kwa wafugaji mnapofanya mikutano…wala hatufurahii wananchi kutozwa faini hizi kwa makosa ambayo pengine yanatokana na kutokujua sheria…” DED Pandawe alifafanua.
Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu Chama cha Wafugaji Tanzania Kusundwa Wamalwa amebainisha changamoto wanazopitia wafugaji ikiwemo kukosekana kwa maeneo ya malisho kutokana na maeneo mengi kuwa hifadhi za misitu hali inayopelekea wafugaji kulazimika kuingia hifadhini, na pia wafugaji kutokuwa sehemu ya maamuzi pale sheria zinapotugwa badala yake wafugaji wanaletewa kuzitekeleza huku akishauri wafugaji wahusishwe katika utunzi wa sheria na miongozo kwa kuwa wao ndio walengwa wakuu.
Na.Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa