WAFANYAKAZI KUPANDA MADARAJA.
SERIKALI kuwapandisha daraja wafanyakazi wote wanaostahili kupanda daraja kwa kuzingatia taratibu na sheria za nchi.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri alipokuwe mgeni rasmi kwenye sherehe za maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi Duniani ambapo wilayani hapa ziliazimishwa katika viwanja vya TASSAF. Pia zilihuzuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sikonge Mhe. Peter Nzalalila pamoja na wafanyakazi wa sekta zote katika Halmashauri ya Sikonge.
Akizungumzia swala la maslai ya watumishi Magiri alisema kuwa serikari imejipanga vizuri kuhakikisha watumishi wote wanaostahili kupanda madaraja wanapandishwa madaraja hayo huku akisisitizia kuhusu watumishi kulipwa madai yao kwa wakati kwani kitendo cha kulimbikiza madai kinaleta dosali katika utendaji kazi. Huku akigusia kuwa watumishi wote wanaohamishwa vituo vyao vya kazi walipwe kwanza garama za kuamishwa na sio kupeleka mtumishi kituo kingine cha kazi bila kumjali ataishi vipi.
Kuhusu swala la rushwa mgeni rasmi alisema kuwa ni marufuku kwa mtu yeyote awe mtumishi au sio mtumishi kujihusisha na swala la rushwa kwani ni adui wa maendeleo huku akiwataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujituma kwani maendeleo ya Taifa la Tanzania yanategeme uwajibikaji wa kila mwananchi.
Mgeni rasmi Mhe. peres Magiri akisikiliza maelezo kwenye banda la idara ya Kilimo siku ya maazimisho ya mei mosi
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bi. Martha Luleka alikemea kitendo cha baadhi ya watumishi kuonekana katika nyumba vinakouzwa vilevi muda wa kazi na kusema kuwa yeye kama mwajili hatokubali kutiwa doa na watumishi wote wa namna hiyo. Huku akiongeza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watumishi wa namna hiyo ikiwemo kukabidhiwa hati ya utumishi goigoi ambavyo watakabidhiwa hadharani ili kuwaumbua.
Pamoja na kuwapongeza wafanyakazi waliopo katika Halmashauri yake Bi. Martha aliongeza kuwa mazingira ya Sikonge bado ni rafiki kwa watumishi kwani yanawawezesha kumudu gharama za maisha kutoka mwezi mmoja hadi mwezi mwingine, huku akiwaasa watumishi wenye jinsia ya kiume kuweka wazi mishahara kwa wenzi wao ili kusaidia ustawi wa familia kwani kumekuwa na desturi ya wanamme kuficha mapato yao jambo linalokwamisha maendeleo ya familia.
Akitoa pongeze zake kwa niaba ya Madiwani Wilayani Sikonge Mhe. Nzalalila alisema kuwa watumishi wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kutoa huduma bora kwa wananchi na kwa wakati huku akiongezea kuwa waendelee kuwa na lugha nzuri kwa wananchi wao na pia wawe na ubunifu katika nafasi walizokabidhiwa.
Sherehe hizo zilipambwa na burudani mbalimbali ikiwemo vikundi vya nyimbo pamoja na maonesho ya kazi za kila idara ambapo katika idara ya maendeleo iliyomtoa mfanyakazi bora Bi. Alice Frank alielezea kuwa wanalengo la kuboresha maisha ya wananchi kwa kutoa mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu ambapo katika hilo mgeni rasmi alisema kuwa ni vizuri kiwango cha mkopo kikaongezwa kwani lengo ni kuwanyanyua wananchi wote na sio wafanyakazi pekee.
Akitoa shukrani zake kwa niaba ya wafanyakazi mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa bwana Nasoro alisema kuwa wanaipongeza serikali kwa kuwajari watumishi huku akiomba malalamiko yote ya watumishi kufanyiwa kazi ikiwemo kupanda madaraja na kulipwa malimbikozo yao kwa wakati.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA TEKINOLOJIA HABARI NA MAWASILIANO
SIKONGE
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa