Maafisa waandikishaji orodha ya wapiga kura wapatao 418 wamepatiwa mafunzo kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024. Mafunzo haya yamejikita mahususi katika kutoa maelekezo muhimu kabla, wakati, na baada ya uandikishaji, huku yakizingatia kanuni,sheria na taratibu za nchi.
Mbali na mafunzo hayo, maafisa hao wamekula kiapo cha uadilifu, ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa haki na uaminifu. Aidha, miongoni mwa maudhui muhimu ni kuzingatia haki na wajibu katika maeneo yote ambapo zoezi litaendeshwa, ili kuimarisha mchakato wa uchaguzi na kuondoa uwezekano wa migogoro.
Msimamizi wa uchaguzi msaidizi, Bw. Geoffrey Mwilawa, amesisitiza umuhimu wa waandikishaji kuelewa kwa kina kanuni na sheria zinazoongoza uchaguzi huu, akionya dhidi ya vitendo vinavyoweza kusababisha taharuki katika utekelezaji wa zoezi hili. Hatua hii ni muhimu ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi na ufanisi, huku ukiwa na thamani ya demokrasia katika jamii.
Zoezi la uandikishaji litaanza tarehe 11 Oktoba hadi tarehe 20, 2024 katika kata zote 20,vijiji 71 na vitongoji 287.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa