Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian ameongoza mkutano wa wadau kujadili utekelezaji wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi mkoa wa Tabora uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Utumishi wa Umma Manispaa ya Tabora.
Akifungua mkutano huo Mhe. Burian amesema changamoto kubwa katika maeneo mengi nchini ni migogoro ya ardhi,hivyo kupitia mkutano huo na mpango wa Serikali wa kutekeleza mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto hiyo nchini hususani kwa mkoa wa Tabora.
Kwa upande wake mratibu wa mradi huo Bw.Joseph Shewiyo amesema ni Halmashauri 37 tu ndio zilizonufaika na mradi huu mpaka sasa. Ameongeza pia kuwa kwa mpango wa mradi huu hakuna mwananchi ambaye atakwenda kulipia gharama yoyote kupata hati ya milki ya ardhi kijijini.
Mkutano huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali toka wilaya ya Sikonge wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha,Katibu Tawala Wilaya ya Sikonge Ndg. Andrea Ng’hwani,Maafisa Tarafa,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe,Waheshimiwa Madiwani,Mwakilishi wa Mhe. Mbunge wa Jimbo la Sikonge pamoja na Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa