VIONGOZI WA WILAYA WACHIMBA MSINGI
Mkuu wa wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri ashiriki kuchimba msingi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya sikonge ikiwa ni jitihada za kuiunga mkono serikari ya awamu ya tano.
Kampeni hiyo iliyoandaliwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Sikonge Mhe. Peter Nzalilila ilifanyika katika eneo maaalum lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya ambalo lipo kijiji cha Mlogolo kata ya Sikonge.
Watu mbali mbali walishiriki katika uchimbaji huo akiwemo mwenyekiti wa CCM, Wilaya, Waheshimiwa madiwani, viongozi wa dini pamoja na wananchi wa Sikonge.
Akizungumza na wananchi hao Mkuu wa Wilaya alisema kuwa pesa zilizotolewa na Selikari ambazo ni kiasi cha Tsh. Bilioni 1.5 zinatakiwa kutumika kwa umakini mkubwa vilevile aliwahasa wananchi kushiriki kwa kujitolea nguvu kazi, kwani mradi huu umeletwa kwa wanachi hao na unalenga kuwanufaisha wana Sikonge na watanzania wote kwa ujumla.
Wananchi wa Sikonge wakishiriki kuchima Msingi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
Wananchi pia walikuwa na neno la shukrani ambapo dua maalum ilisomomwa na shehe aliyewaombea viongozi wote kuendelea kuwa na hekima na kuwaongoza katika kufanya mambo mema na yenye tija katika nchi hii. Sanjari na hayo pia waliiombea amani ya nchi na kumuweka Mhe. Raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mikononi mwa Mungu ili azidi kuwakumbuka watanzania wengi wenye hali ya chini jambo ambalo amekuwa akilifanya tokea ameingia madarakani.
Akitoa neno la shukrani kwa wote waliofika Mhe. Nzalalila alisisitiza vijana kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili wanufaike na miradi inayoletwa katika Halmashauri yao. Sambamba na hilo pia alipeleka neno la shukrani kwa mbunge wa Jimbo la Sikonge Mhe. Joseph Kakunda kwa kuendelea kuwakumbuka wananchi wake na kupigania maendeleo yao ili kutimiza ilani ya uchaguzi ya CCM.
IMEANDALIWA NA
KITENGO CHA TEKINOLOJIA HABARI NA MAWASILIANO
SIKONGE.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa