Na Linah Rwambali
Mbunge wa Jimbo la Sikonge Mhe. Joseph Kakunda amezindua shule ya Msingi Kininga iliyopo katika Kata ya Ipole.
Akizungumza wakati wa tukio hilo Mhe. Kakunda alisema anaishukuru serikali kwa kuwapa fedha kwaajili ya ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa na ukarabati wa shule hiyo kwani hapo awali watoto walikuwa wanatembea umbali mrefu kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa kwenda shule ambazo ziko mbali na makazi yao hali iliyokuwa inaathiri ufaulu wa watoto hao.
“Ninamshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupokea maombi ya kukarabati na kuongeza vyumba vya madarasa katika shule hii ambayo nilimpelekea mnamo mwaka 2021. Baada ya kumwelezea hali ya shule aliamua kutoa fedha kwaajili ya kujenga vyumba vipya nane vya madarasa vitakavyotosheleza idadi ya watoto waliopo pamoja na matundu sita ya vyoo, hatimaye sasa imekamilika” alisema.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Mgope alimshukuru Mhe. Kakunda kwa kuendelea kuwasilisha changamoto zao na kuwataka wananchi watunze miundombinu hiyo waliyotengenezewa na serikali.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa