Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani leo tarehe 1 Agosti, 2017 amezindua mradi wa umeme vijijini REA awamu ya tatu katika Mkoa wa Tabora. Ambapo uzinduzi huo umefanyika katika kata ya Kisanga Wilayani Sikonge, aidha ameliagiza Shirika la umeme TANESCO kumsimamia vizuri mkandarasi aliepewa kazi hii ya kusambaza umeme vijijini ili kila nyumba ipate umeme kwa wakati. Aidha, Naibu Waziri amesisitiza kuwa nyumba zote hata za nyasi zitapata umeme na gharama ya kuunganishiwa umeme ni Tsh. 27,000/= elfu tu. Pia Naibu Waziri amesema, mradi huu wa REA awamu ya tatu una kazi zifuatazo:-
Aidha, Naibu Waziri amewakabidhi na kuwaagiza wakandarasi kumaliza kazi hiyo ndani ya miezi 18 ili miezi 6 iwe ya kufanya marekebisho madogomadogo tu. Pia amesisitiza kuwa hatowaongeza muda wakandarasi hao wasipo maliza kazi hiyo ndani ya muda bali atashikilia mishahara yao.
TANESCO pia wameagizwa kuweka kituo chao katika kata ya Kisanga ili wateja wasipate shida ya kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kufanya malipo ya kuunganishiwa umeme na ikibidi wao TANESCO ndio wawafuate wateja huko walipo. Mhe. Dkt. Medard Kalemani alisema mwananchi apate umeme ndani ya wiki moja baada ya malipo na kusiwe na mizunguko isiyona sababu kumsumbua mwananchi.
HAPA KAZI TU- AGOSTI 2017
Imeandaliwa na Kitengo cha TEHAMA, Sikonge.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa