Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Bi. Faraja Hebel ameongoza uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya sheria yaliyofanyika katika Viwanja vya Tasaf -Sikonge.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Sikonge,Mwakilishi wa Mwendesha Mashtaka Mkoa wa Tabora, Afisa Ustawi wa Jamii na Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Sikonge.
Akizindua maadhimisho hayo Bi. Faraja amesisitiza umuhimu wa wananchi kufahamu sheria hata kwa uchache ili kuwa raia wema na kuepuka ukiakaji wa sheria za nchi.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Sikonge Mhe. John Mpitanjia Mnamba amepongeza kufanyika kwa maadhimisho hayo na kuahidi ufanisi mkubwa kwa maadhimisho yajayo ikizingatiwa kuwa maadhimisho hayo yamefanyika kwa mara ya kwanza kwani hapo kabla hayakuwahi kufanyika kwa sababu ya kutokuwepo kwa Mahakama ya Wilaya hapa Sikonge.
Maadhimisho hayo yanalenga kuongeza uelewa wa sheria kwa wanachi ili kujenga jamii ya watu wanaofahamu sheria za nchi yao na kuzifuata.Shughuli zitakazofanyika katika wiki ya sheria ni pamoja na utoaji huduma za kisheria katika shule zote za kata ya Sikonge pamoja na Ofisi za Wenyeviti wa vitongoji kuanzia Januari 27 hadi Januari 31 ,2024 ambapo itakuwa ni siku ya kilele cha maadhimisho hayo.
Akihitimisha maadhimisho hayo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Mhe. Winfrida Magai amewashukuru wote waliohudhuria uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria “Tunawashukuru sana kwa kuitikia wito wetu,Madam Faraja kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Sikonge,Asante sana tunakushukuru kwa kutuheshimu na kuweza kutufungulia wiki yetu ya sheria.Lakini pia nikushukuru Kaimu Mkurugenzi Bw.Kayange kwa kuweza kujumuika pamoja nasi na kipekee pia nikushukuru Kaimu Kamanda wa Polisi Wilaya ya Sikonge ambaye pia ni mkuu wa kituo cha polisi Sikonge” Amesema Mhe. Magai.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa