Katibu Tawala wa mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya amefanya ziara ya kawaida wilayani Sikonge kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2023/2024.
Katika ziara hiyo Dkt. Mboya ametembelea ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ibaya inayojengwa kwa fedha toka serikali kuu shilingi milioni 50,ujenzi umefikia asilimia 60 ya utekelezaji.
Vilevile amekagua ujenzi wa matundu 15 ya vyoo katika shule ya msingi Mitowo inayojengwa kwa fedha za mfuko wa wahisani (SWASH) shilingi milioni 45.7,ujenzi umefikia asiliami 98 ya utekelezaji.
Mradi mwingine uliotembelewa na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora ni ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mkolye,unaojengwa kwa fedha toka serikali kuu shilingi milioni 138,ujenzi umefikia asilimia 90 ya utekelezaj, ambapo Dkt. Mboya amepongeza juhudi za Mkurugenzi pamoja na diwani wa kata ya Mkolye Mhe.Omar Kategile pamoja na kamati ya ujenzi kwa ufuatiliaji na uwepo wao wakati wote wa mradi unapotekelezwa.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bi. Tausi Yunge amesisitiza kuzingatia ufungaji wa mifumo ya Tehama katika zahanati zinazojengwa pamoja na vituo vya afya. “Tuzingatie ufungaji wa mifumo ya Tehama katika zahanati zetu,mara nyingi tunatengeneza tu mifumo ya umeme na kusahau kuandaa mifumo ya Tehama hususani mfumo wa GOTHOMIS.”amesema Bi. Yunge.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Nico Kayange amemshukuru Dkt. Mboya kwa kufika Wilaya ya Sikonge na ameahidi kwenda kuyafanyia kazi yale yote yaliyoshauriwa na wataalam toka ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora.
Akihitimisha ziara hiyo Dkt. Mboya amesisitiza watalaam wa halmashauri kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo kwa ustadi ili thamani ya fedha zinatoletwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ionekane.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa