Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe amewakumbusha watumishi wa umma kuwa watiifu kwa mamlaka na kufuata kanuni,sheria na taratibu za utumishi wa umma pale wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.
Ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na watumishi wa kada mbalimbali wa ajira mpya katika kikao kazi kilichoandaliwa na divisheni ya utawala na usimamizi wa rasilimali watu katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri.
Naye Mkuu wa divisheni ya utawala na usimamizi wa rasilimali watu Bw. Nico Kayange amesisitiza watumishi kufuata maelekezo ya serikali kwa kuepuka kufanya mambo yatakayosababisha kuvujisha siri za serikali ikiwa ni pamoja na kufanya kazi zao katika maeneo ambayo mambo ya serikali yatabaki kuwa siri,hasa shughuli zinazofanyika kupitia mifumo ya Tehama. “Watumishi wa umma mnawajibu wa kuzingatia utunzaji wa siri za serikali,msifanyie kazi zenu kwenye stationery za mitaani,nenda kwenye taasisi ya umma iliyo karibu na wewe kutekeleza shughuli zako.”amesema Bwana Kayange.
Kikao kazi hicho kimemulika mambo muhimu ya kuzingatia kwa watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na muongozo wa mavazi kwa watumishi wa umma,haki na wajibu wa mtumishi wa
umma pamoja na majadiliano amabyo yamewapa watumishi wasaa wa kuuliza mambo mbalimbali ya kiutumishi yaliyohitaji ufafanuzi kutoka kwa mwajiri.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa