UKAGUZI
Mkuu wa wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Mgiri atembelea ujenzi wa hospitali ya Wilaya unaoendelea sikonge.
Magiri alifika eneo hilo ili kujionea hatua iliyofikiwa na namna utendaji kazi unavyoendelea. Sanjari na kuangalia changamoto zozote zinazoweza kukwamisha ujenzi kuendelea kwa kasi iliyokusudiwa.
Mhe. Magiri alimuagiza Muhoro Traders kuhakikisha anafanya kazi kwa bidii ili kufikia Malengo kwa kuzalisha tofali kwa idadi sawa na mkataba unavyosema wa tofali elfu tatu kwa siku.
Kama ilivyo ada ya viongozi mbali mbali wilayani Sikonge kutembelea na kusimamia miradi yote inayoendeshwa katika halmashauri hii. Naye mkurugenzi alisisitiza mafundi wote waliopewa tenda ya ujenzi kuwahi kazini kwa wakati ili shuguli zote zifanyike kwa wakati huku akikemea baadhi ya vibarua kuacha uvivu kwenye kazi.
Mbali na hayo pia Mkurugenzi Mtendaji (W) Sikonge Bi. Martha Luleka pia alitoa maagizo kuhakikisha kuwa kampuni iliyopewa kibali cha kuzalisha tofali inaleta mashine mbili za kuzalisha tofali ili kuweza kuzalisha idadi kubwa ya matofali na kuacha kukwamisha ujenzi wa Hospitali na kuendelea na kasi.
Msingi wa jingo la Wagonjwa Wa nje (OPD) hospitali ya Wilaya ya Sikonge .
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa