TUNAOMBA TUPATIWE MAFUNZO YA KIUTUMISHI YATUSAIDIE KUTUJENGEA UWEZO WA KUHUDUMIA JAMII" WATENDAJI SIKONGE.
Watendaji wa Kata na Vijiji Wilayani Sikonge wameomba kupatiwa mafunzo ya kiutumishi yanayoendana na wakati ili waweze kutekeleza majukumu yao.
Watumishi hao wameyasema hayo mbele ya Mkurugenzi ambae ameendelea na ziara katika kata za; Kipanga, Kiloleli na Usunga na kuongeza kuwa kwa kupatiwa semina/mafunzo mbalimbali yatawajengea uwezo wa kiutumishi ili waweze kutatua changamoto na kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa ufanisi.
"Tunaomba tupatiwe semina kuna masuala ya kisheria mengi ambayo tunashindwa kuyatatua kutokana na kutokujua sheria na taratibu mbalimbali hali inayopelekea kufanya maamuzi mengine ambayo si sahihi kulingana na wakati ..." Mtendaji kata ya Kipanga.
Aidha,Kaimu Mkurugenzi ambae pia Ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu(W) Nico Kayange amesema atalifanyia kazi ombi hilo kwa kuwa ni muhimu kwa ustawi wa watumishi huku akiwashauri watumishi kujiendeleza kielimu ili waongeze ufanisi katika utendaji wao.
Sambamba na hilo Ndg. Kayange ameahidi kutatua changamoto na kero zote ambazo watumishi hao wamezitoa akishirikiana na menejimenti nzima ili kwa pamoja waweze kufanya kazi katika mazingira bora na rafiki huku akiwataka watumishi wote kufanya kazi kwa weledi wakizingatia sheria na taratibu za utumishi wa Umma.
Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa