• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Sikonge District Council
Sikonge District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Idadi ya Watu
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Mifugo na uvuvi
      • Afya na Ustawi wa jamii
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mazingira na Taka ngumu
      • Kilimo, Umwagilaji na Ushirika
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Uchimbaji wa Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo Ndogo
    • Miongozo Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya sanaa
      • Sanaa za picha
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba
    • Habari mpya
    • Matukio

TUMIENI MIKATABA YA KISHERIA KUWABANA WAKULIMA ILI WASITOROSHE TUMBAKU

Imewekwa: June 14th, 2019

TUMIENI MIKATABA YA KISHERIA KUWABANA WAKULIMA ILI WASITOROSHE TUMBAKU

NA EVELINA ODEMBA

VIONGOZI wa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) wilayani kuingia mikataba ya kisheria na wanachama wao ili kuwabana wasitoroshe tumbaku na kusababishia deni.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri wakati akifungua mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta ya tumbaku ambao uliwahusisha Madiwani , Viongozi wa AMCOS na Wawakilishi kutoka Kampuni za ununuzi wa tumbaku.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Sikonge alisema hatua hiyo itasaidia kuuwachukulia hatua za kisheria viongozi na wanachama wanaobainika kukiuka taratibu za vyama ikiwemo kutorosha tumbaku na kuuza kwa njia ya magendo.

Magiri aliongeza kuwa vitendo vya namna hiyo vimesababisha baadhi ya AMCOS kufa kwa sababu ya kuwa na madeni na kushindwa kupata makisio ya kilimo cha tumbaku.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wanunuzi wa tumbaku kuhakikisha wanafanya mapema malipo ya wakulima ili kuepuka utoroshaji wa tumbaku kwa ajili ya kutafuta fedha za haraka za kusaidia familia zao.

Magiri alizitaka Benki kuidhinisha mikopo ya vyama vya msingi kwa wakati ili kumwezesha msambazaji kusambaza pembejeo kwa wakati.

Akisoma maazimio ya mkutano huo kwa niaba ya wadau wa sekta ya tumbaku Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Peter Mihayo Nzalalila alisema wataandika barua kwenda kwa Waziri wa Kilimo kuomba kuongezewa madaraja ya tumbaku kwa sababu uwepo wa madaraja machache umesababisha mkulima kunyonywa.

Alisema wamekubaliana kuwa Vyama vya msingi viwasaidie wakulima wao kujikomboa kiuchumi kwa kuwapa makisio ambayo yapo ndani ya uwezo wao.

Nzalalila aliongeza Vitabu vya sheria vya Bodi ya tumbaku vitafsiriwe katika lugha ya Kiswahili na kugawiwa kwa viongozi wa vyama vya msingi ili viwasaidie wanachama wote kujua haki zao za msingi.

Alisema kuwa ni vema mikopo ya pembejeo itolewe mapema mwezi wa Tisa ili wakulima wajiandae mapema kuingia kwenye msimu wa kilimo.

Nzalalila alisema kuwa makisio ya wakulima wa kujitegemea pia yaingizwe kwenye takwimu za ushirika ili wakulima hao wasikose pa kuiuzia tumbaku yao.

Awali akitoa kilio cha wakulima wa tumbaku Mwenyekiti wa Kisanga AMCOS Rashid Mazinge alisema mauzo ya msimu huu yamekuwa mabaya sana kwani wakulima wengi wameuza chini ya wastani wa Dola moja jambo ambalo litasababisha wengi wao kulaza madeni ya pembejeo.

Alisema wateuzi wa Kampuni wamekuwa wakitoa bei ya chini kwa kisingizio kuwa tumbaku ya mwaka huu haina ubora.

Aidha Mazinge alisema kuchelewa kwa mbolea kuwafikia wakulima wengi kumesababishia hasara kubwa wakulima na kupata bei ya chini.


Matangazo

  • TANGAZO LA ZABUNI YA KUKODISHA CANTEEN [MGAHAWA] MPYA KWENYE JENGO LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZAABUNI YA KUMPATA MWEKEZAJI KATIKA KIWANDA CHA KATI CHA KUCHAKATA MAZAO YA NYUKI(MARUDIO) June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA USAFI KWENYE OFISI ZA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA ULINZI June 07, 2023
  • Angalia zaidi

Habari Mpya

  • UZINDUZI WA SHULE YA MSINGI KININGA - KATA YA IPOLE

    May 09, 2025
  • MJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA WILAYANI SIKONGE

    May 07, 2025
  • KIKAO CHA TATHIMINI YA MKATABA WA LISHE WILAYANI SIKONGE

    April 29, 2025
  • WATENDAJI WA INEC WILAYANI SIKONGE WAMEKULA KIAPO CHA UADILIFU, KUJIWEKA KANDO NA VYAMA VYA SIASA.

    April 29, 2025
  • Angalia zaidi

Video

Ziara ya Waheshimiwa Madiwani Wilayani Rungwe - Mbeya.
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Zabuni
  • Matukio
  • Matangazo
  • Habari

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Mkoa wa Tabora
  • TAMISEMI
  • Urambo DC
  • UTUMISHI
  • Kaliua DC

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC

    Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora

    Simu: 0767135460

    Simu: 0767135460

    Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma zetu

Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa