TSH.MILIONI 109 KUJENGA ZAHANATI MWAMAYUNGA.
Mbunge jimbo la Sikonge Mhe.Joseph Kakunda ameendelea na ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo Zahanati ya Mwamayunga iliyopo Kata ya Kisanga na kuwapongeza wananchi kwa kujitolea kwa sehemu Kubwa huku Serikali ikitoa Tsh.Milioni 50 sambamba na Mfuko wa Jimbo Ukichangia Tsh Milioni 8.6."Nimefurahishwa sana na majitoleo ya wananchi,hongereni sana kwa kazi nzuri..mradi ni mzuri na ukikamilika wananchi watapata huduma ya Afya hapahapa..Serikali imeleta fedha ili wananchi wapate huduma zinazotakiwa.."Mhe.KakundaUjenzi wa Zahanati ya Mwamayunga utagharimu Tsh.Milioni 109 na zahanati hiyo inatarajiwa kukamilika na kutoa huduma za Afya ifikapo Januari 2022.Aidha,Mhe.Kakunda ametembelea boma la vyumba viwili vya madarasa na Ofisi moja Shule ya Msingi Shikizi ya Ulyanyama yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi , Zahanati ya Kisanga pamoja na Shule ya Msingi Kisanga.Na.Anna Kapama
Mbunge jimbo la Sikonge Mhe.Joseph Kakunda ameendelea na ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo Zahanati ya Mwamayunga iliyopo Kata ya Kisanga na kuwapongeza wananchi kwa kujitolea kwa sehemu Kubwa huku Serikali ikitoa Tsh.Milioni 50 sambamba na Mfuko wa Jimbo Ukichangia Tsh Milioni 8.6.
"Nimefurahishwa sana na majitoleo ya wananchi,hongereni sana kwa kazi nzuri..mradi ni mzuri na ukikamilika wananchi watapata huduma ya Afya hapahapa..Serikali imeleta fedha ili wananchi wapate huduma zinazotakiwa.."Mhe.Kakunda.
Ujenzi wa Zahanati ya Mwamayunga utagharimu Tsh.Milioni 109 na zahanati hiyo inatarajiwa kukamilika na kutoa huduma za Afya ifikapo Januari 2022.
Aidha,Mhe.Kakunda ametembelea boma la vyumba viwili vya madarasa na Ofisi moja Shule ya Msingi Shikizi ya Ulyanyama yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi , Zahanati ya Kisanga pamoja na Shule ya Msingi Kisanga.
Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa