Sikonge _Tabora
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Seleman Pandawe ameongoza kikao cha Kamati ya Lishe Wilaya na kuwasisitiza ,Afisa Lishe na Idara mbalimbali zilizo katika Kamati hiyo kuhakikisha suala la Lishe hasa Kwa Wanafunzi Shuleni linatiliwa Mkazo ili kujenga Afya ya Jamii.
"Suala la lishe liwe la Kwanza katika bajeti zenu za Idara husika, Mheshimiwa Rais Samia ameweka Mikakati ikiwemo mikataba ya Afua ya Lishe ili kuhakikisha linatekelezwa hadi ngazi ya chini kabisa Kwa wananchi" Ded Pandawe.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa Afua ya Lishe Kwa kipindi cha Julai_Desemba 2022, Afisa Lishe Wilaya ya Sikonge Veronica Frednand amesema pamoja na Mikakati mbalimbali waliyoiweka kuhakikisha Afua hiyo inatekelezwa wamehakikisha kila Idara inayohusika katika Lishe inatenga bajeti Kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake.
Halmashauri inetenga kiasi cha Tsh.Milioni 50 Mapato ya ndani huku Idara ya Elimu Msingi ikisimamia upatikanaji wa Chakula katika Shule 38, Kilimo cha mazao ya Chakula katika Shule 104 Kati ya Shule 108 za Halmashauri hiyo.
Aidha, Idara ya Elimu Sekondari imesimamia Kilimo cha mazao ya Chakula Ekari 51 katika shule 20 Kati ya Shule 22 za Sekondari Wilayani hapo.
Lengo la Mikakati hiyo ni kuhakikisha Chakula Kinatolewa Katika Shule zote za Msingi na Sekondari za Wilaya.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa