SIKU YA UKIMWI DUNIANI YAADHIMISHWA KIMKOA WILAYANI SIKONGE.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Balozi.Dkt.Batilda Buriani amewaongoza wananchi Mkoa wa Tabora katika kuadhimisha siku ya UKIMWI Duniani Kata ya Ipole Wilayani Sikonge na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
Akitoa hotuba katika maadhimisho hayo Balozi.Dkt.Batilda amesema hali ya maambukizi kwa Mkoa wa Tabora imepungua ambapo takwimu zinaonesha ni asilimia 5.1 ya maambukizi kwa mwaka 2021 hali ambayo imechangiwa na uelewa mpana wa watu pamoja na hatua madhubuti zinazochukuliwa kujikinga na maambukizi hayo.
Aidha,Balozi Batilda amepongeza mashirika na taasisi binafsi zinazotoa Elimu ya mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI hatua ambayo imesaidia kupunguza maambukizi hayo.
Sambamba na hilo Balozi Batilda amewasisitiza wananchi hasa vijana kujilinda dhidi ya maambukizi huku akiwaasa kupima ili kujua afya zao.
"..Tuazimie leo kuhakikisha tunafata misingi inayotakiwa..tuwe waadilifu katika kutunza afya zetu, takwimu zinaonesha kundi la vijana wenye umri wa miaka 15-24 wanaongoza kwa maambukizi kuliko makundi yote..lakini pia niwapongeze wale wote ambao wamepima afya zao leo" Balozi.Dkt.Batilda.
Maadhimisho hayo kwa mwaka 2021 yamebeba kaulimbiu isemayo; "ZINGATIA USAWA,TOKOMEZA UKIMWI,TOKOMEZA MAGONJWA YA MLIPUKO"
Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa