SIKONGE YAPOKEA MSAADA WA REFLECTIVE JACKET KUTOKA UBALOZI WA OMAN NCHI TANZANIA.
Ubalozi wa Oman nchini Tanzania watoa msaada wa Reflective Jacket kwa Mkuu wa Wilaya ya Sikonge.
Akipokea msaada wa jumla ya Reflective Jacket mia mbili (200) Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri alitoa shukrani kwa Balozi wa Oman Mhe. Salum AL-Mahrooqy kwa msaada huo na kusema ni imani yake kuwa unatokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Oman.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri mwenye shati ya kijani pamoja na KUU ya Wilaya na wa wawakilishi wa Ubalozi wa Oman wakiwa katika picha ya pamoja wakati msaada ukitolewa.
“kwa niaba ya serikali, Wilayani Sikonge tumepokea msaada wa Reflective Jacket 200 kutoka kwa Balozi wa Oman ambazo zitatumika kuwasaidia askari wa usalama Barabarani” alisema Mkuu wa Wilaya.
Jacket hizo zinategemewa kukabidhiwa kwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Sikonge ili awakabidhi askari wa usalama barabarani.
Msaada huo uliokabidhiwa na Mzee Hemed Nassor kwa niaba ya Balozi wa Oman nchini Tanzania ambapo aliambatana na familia yake na kukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa