Tume huru ya taifa ya uchaguzi imeendesha mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga Kura wilayani Sikonge kwa maafisa waandikishaji wasaidizi na maafisa waendeshaji wa vifaa vya Bayometriki (BVR) zaidi ya mianne ambao wanatarajiwa kutekeleza zoezi hilo katika kata ishirini zilizopo katika jimbo la Sikonge.
Akizindua mafunzo hayo Afisa muandikishaji wa jimbo la Sikonge Ndg.Benjamin Mshandete amesema maandalizi yanaendelea vizuri na washiriki wote walioteuliwa na tume katika jimbo la Sikonge wanapatiwa Mafunzo ya uboreshaji wa daftari ikiwemo matumizi ya BVR katika uingizaji wa taarifa na utoaji wa vitambulisho kwa raia watakaokwenda kupata huduma.
Aidha Mshandete amewataka Watendaji wa vituo vya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga Kura kushirikiana katika utunzaji wa vifaa vya BVR ili wananchi wote watakaojitokeza waweze kupata huduma kama ilivyokusudiwa na serikali.
Kwa upande wake Afisa kutoka TAKUKURU Bw.Homboyo Mathias amewataka maafisa waandikishaji wasaidizi na maafisa waendeshaji kuzingatia viapo vyao katika utendaji kazi wao ikiwemo kusimamia maadili na kuepuka rushwa .
Naye Mwenyekiti wa watendaji wa vituo vya uboreshaji Joseph Kavishe amesema elimu na ujuzi wanaopatiwa utawasaidia kufanya kazi kwa weledi na ufanisi ikiwemo kutumia kwa usahihi vifaa vya kisasa vya BVR.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanaendelea katika Ukumbi wa Halmashauri , Chuo cha Wananchi FDC na Shule ya sekondari Kamagi.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa