SIKONGE KUJIPATIA HOSPITALI YA WILAYA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bi. Martha Luleka atembelea ujenzi wa jengo la Hospitali ya Wilaya ya Sikonge
Ikiwa ni ziara yake ya mara kwa mara katika mradi huo awamu hii Bi. Martha alikutana na baadhi ya mafundi ambao alizungumza nao kuhusu mambo mbali mbali yanaokabili ujenzi wa Hospitali hiyo lakini kubwa kuliko likiwa ni namna mafundi wanavyoweza kukamilisha kazi zao kwa wakati
Alipokuwa akikagua jengo la mama na mtoto Mkurugenzi alizungumza na fundi Alphonce Mtewa ambaye pia ndio msimamizi wa jengo hilo ambapo alishauriwa kuongeza idadi ya mafundi na wasaidizi kwani kutumia rasilimali watu ndogo inachelewesha kazi na pia ni utumiaji wa garama kubwa na upotezaji wakati. Fundi huyo aliahidi kufanyia kazi agizo hilo
Sanjari na hayo pia kwenye jengo la madawa injinia Rajabu Ismail aliahidi kuonesha mabadiliko makubwa ili kuendana na kasi ya muda. Akipokea ushauri uliotolewa na Mkurugenzi pia aliomba kupewa siku mbili kuukamilisha msingi na kuinua jengo.
Bi. Martha pia alitoa pongezi kwa mafundi kutokana na moyo wao wa kujituma kwani baadhi yao walikutwa wakifanya kazi hadi usiku, jambo lililoonesha kuwa kweli wana uzalendo na nchi yao na pia baadhi wamekuwa wakijitolea kusogeza tofari eneo la jengo bila malipo yeyote.
Ikumbumbukwe kuwa Wilaya ya Sikonge ilipokea shilingi za kitanzania Bil. 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambapo kwa hatua ya kwanza yanategemewa kujengwa majengo saba. Hii ikiwa ni miongoni mwa utekelezaji wa ilani ya CCM ambayo pia ililenga kuboresha huduma za afya ambayo ni pamoja na kusogeza huduma hizo karibu na wananchi. Hivyo basi Wilaya ya Sikonge ni miongoni mwa Wilaya zitakazonufaika na jambo hilo.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA TEKINOLOJIA HABARI NA MAWASILIANO(TEHAMA)
SIKONGE.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa