• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Sikonge District Council
Sikonge District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Idadi ya Watu
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Mifugo na uvuvi
      • Afya na Ustawi wa jamii
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mazingira na Taka ngumu
      • Kilimo, Umwagilaji na Ushirika
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Uchimbaji wa Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo Ndogo
    • Miongozo Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya sanaa
      • Sanaa za picha
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba
    • Habari mpya
    • Matukio

SERIKALI YAONYA WAVAMIAJI WA MISITU

Imewekwa: June 6th, 2019

SERIKALI YAONYA WAFUGAJI WANAOVAMIA MISITU YA HIFADHI.

Na Evelina Odemba

SERIKALI yapiga marufu  wakulima na wafugaji kuvamia eneo la Misitu ya hifadhi na kufanya shuguli zao kwenye misitu hiyo.

Hayo yalibainishwa na ,Meneja wa kanda wa wakala wa misitu (TFS) bwana Valentine Msusa alipokuwa akizungumza na wakazi wa kata ya Kipili iliyopo Wilayani Sikonge katika mkutano wa hadhara uliohuzuliwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa, kamanda wa Polisi Mkoa, na Mkuu wa Wilya ya Sikonge aliyekuwa mwenyeji wa mkutano huo.

Aidha bwana Msusa alionya wafugaji wote wanaovamia maeneo ya hifadhi na kujimilikisha maeneo hayo kinyume cha utaratibu uliowekwa kuwa watapigwa faini huku akiweka bayana kuwa kfugaji atakayekutwa na mifugo yake ndani ya hifadhi atakuwa amevunja makosa matatu kwa pamoja hivyo atatozwa faini  isiyopungua laki tatu mpaka milioni tisa kwa makosa hayo.

Hata kivyo katibu Tawala wa Mkoa Mhe. Musalika Makungu alisema kuwa lengo la serikali sio kutoza faini bali kuhakikisha taratibu zilizowekwa zinafuatwa huku akongeza kuwa serikali inawatambua wafugaji kama sekta muhimu inayochangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi. Hivyo basi kwa thamani hiyo Wilayani Sikonge kumetengwa eneo maalum litakalokodishwa kwa wafugaji kwa shuguli za malisho  huku akiitaja sehemu ya hifadhi ya Ipembampanzi kutengwa kwa shuguli hiyo.

“sio jambo la kufurahisha kuwa mfugaji anayepigwa faini mara kwa mara, mimi mwenyewe ni mfugaji wa siku nyingi ninayefuga kwa kufuata utaratibu”, alisema na kuongeza kuwa wakati wa kufuga mifugo mingi umepitwa na wakati na kuwataka wafugaji kwenda na wakati wa kufuga mifugo michache watakayoweza kuihudumia kwa malisho.

Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri akizungumza na wananchi wa kata ya Kipili alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara.

Aliyasema hayo alipokuwa akijibu swali la mfugaji Didia Mapowogo aliyetaka kujua lengo la serikali kuhusu kuongeza eneo la kuchungia kwani eneo lililotengwa ni dogo kulinganisha na idadi ya mifugo inayopatikana eneo la Kipili pekee.

Naye Mkuu wa Wilaya Mhe. Peres Magiri aliwataka wananchi wilayani kwake kutii sheria bila shuruti. Huku akifafanua kwa wakulima ambao mazao yao yapo katika maeneo ya hifadhi kujiandikisha kwa uongozi wa kata ili wapewe muda wa kuyavuna na kusisitiza kuwa baada ya kuvuna hakuna mkulima au mfugaji atakayeruhusiwa kuingia kwenye maeneo ya hifadhi bila kibali.

Matangazo

  • TANGAZO LA ZABUNI YA KUKODISHA CANTEEN [MGAHAWA] MPYA KWENYE JENGO LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZAABUNI YA KUMPATA MWEKEZAJI KATIKA KIWANDA CHA KATI CHA KUCHAKATA MAZAO YA NYUKI(MARUDIO) June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA USAFI KWENYE OFISI ZA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA ULINZI June 07, 2023
  • Angalia zaidi

Habari Mpya

  • UZINDUZI WA SHULE YA MSINGI KININGA - KATA YA IPOLE

    May 09, 2025
  • MJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA WILAYANI SIKONGE

    May 07, 2025
  • KIKAO CHA TATHIMINI YA MKATABA WA LISHE WILAYANI SIKONGE

    April 29, 2025
  • WATENDAJI WA INEC WILAYANI SIKONGE WAMEKULA KIAPO CHA UADILIFU, KUJIWEKA KANDO NA VYAMA VYA SIASA.

    April 29, 2025
  • Angalia zaidi

Video

Ziara ya Waheshimiwa Madiwani Wilayani Rungwe - Mbeya.
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Zabuni
  • Matukio
  • Matangazo
  • Habari

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Mkoa wa Tabora
  • TAMISEMI
  • Urambo DC
  • UTUMISHI
  • Kaliua DC

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC

    Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora

    Simu: 0767135460

    Simu: 0767135460

    Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma zetu

Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa