SENSA YA MIFUGO NI MUHIMU.
Wafugaji waaswa kubadili mfumo wa ufugaji kuwa wa kisasa ili waweze kunufaika na mifugo wanayoihudumia.
Akizungumza na wananchi na wafugaji wa kata ya Ngoywa wilayani Sikonge, mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Peter Nzalalila alisema kuwa ufugaji wa sasa unahitaji kufuata njia za kitaalamu ili kuvuna mazao mengi ya mifugo ambayo ni Nyama na Maziwa kwani lengo ni kila mfugaji awe na maisha bora na mifugo bora yenye kuteka soko.
Akiongelea zoezi la Sensa ya mifugo Mhe. Nzalalila alisema kuwa zoezi hilo ni muhimu kwani litasaidia serikali kutenga maeneo sahihi kwa ajili ya kulishia mifugo. Hivyo basi wafugaji wanapashwa kuliunga mkono kwa jihudi zote.
Wananchi na Wafugaji wa Ngoywa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sikonge Mhe. Peter Nzalalila.
Akichangia swala hilo Mtendaji wa Kata ya Ngoywa Bi. Sabina aliwaomba wakulima kubadilika na kuondoka na mila potofu ya kutoa idadi pungufu ya mifugo tofauti na idadi kamili ya mifugo waliyonayo kwani wamekuwa na utamaduni wa kuficha baadhi ya mifugo wakiamini kwa kufanya hivyo watakwepa kuchangia michango mbali mbali ya mifugo yao.
Naye Afisa Mifugo Wilaya Bwana Gerad Mwagalazi aliwahasa wafugaji kutoingiza siasa kwenye swala muhimu kama sensa ya Mifugo nakwani ni kwaajili ya maendeleo yao aliongeza, “mfugo unataka eneo Fulani kwa mwaka tuupe haki yake kwa kutoa takwimu halisi” akisisitizia hilo pia alisema kuwa serikali itakapowapangia wafugaji maeneo ya kulishia itategemeana na takwimu zilizotoleawa. Huku akisema kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni zuri na linalenga kusaidia makundi yote ambayo yalikuwa yamesahaulika kipindi cha nyuma hivyo basin a wafugaji waiunge mkono.
Mbali na kutoa elimu pia alikemea kitendo kinachofanya na baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo ndani ya hifadhi kwani watakapobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupigwa faini. Ambapo wafugaji walikubali kushiriki sense huku wakiahidi kuwahamasisha na wengine ambao hawakushiriki kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa