RC BALOZI BURIANI AUAGIZA UONGOZI WILAYANI SIKONGE KUWAONDOA WATOTO WANAOISHI ENEO HATARISHI KATIKA MGODI WA KITUNDA.
Na.Anna Kapama
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Sikonge kuwaondoa watoto wanaoishi katika eneo la uchimbaji madini Kitunda baada ya kubaini kuwa wameanzisha kibanda na kufundisha watoto hao katika eneo hatarishi kwa usalama wao.Balozi Dkt. Batilida ameyasema hayo baada ya kutembelea eneo hilo kwa ajili ya kujionea Kibanda kilichojengwa katika eneo la Mgodi kwa kutaka kukigeuza Shule ya Msingi kinyume na utaratibu wa kuanzisha shule na kuongeza kuwa Kibanda hicho kilipojengwa ni hatari kwa afya za watoto kwa kuwa kipo karibu eneo la kuchanganyia kemikali kwa ajili ya kuchenjulia dhahabu na pembeni yake kuna shimo lenye maji yenye kemikali hatari zinatumika kusafishia dhahabu ambazo ni hatari kwa maisha ya bianadamu.
Aidha Balozi Dkt Batilda amesema hakuna sababu ya kuanzisha kibanda hicho mgodini kwani kuna eneo la kijiji ambalo wangeazisha shule kwa kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inatoa shilingi milioni 900 kila mwezi kwa ajili ya elimu bure Mkoani Tabora.
Katika hatua nyingine Balozi Dkt. Batilida ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kukagua maeneo yote ya misitu inayopo wilayani hapo ili kuhakikisha hakuna wananchi wanaoishi na kuendesha shughuli za kibinadamu kinyume cha Sheria huku akiwaagiza Ofisi ya Madini kukagua migodi yote ya Mkoa wa Tabora ili kuhakikisha hakuna vitendo ambavyo vinakiuka sheria na taratibu za uchimbaji madini.Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo amesema wameanza kuchukua hatua stahiki kuhakikisha watoto wote wanaondolewa eneo hilo na kuwapeleka katika kijiji jirani ili wapate elimu kwenye mazingira salama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa