RAS AKAGUA HOSPITALI YA SIKONGE
KATIBU tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu atembelea ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Sikonge ili kujiridhisha namna ujenzi unavyofanyika.
Akiwa katika jengo la mama na mtoto Msalika alishauri mafundi kuongeza nguvu kazi ikiwemo muda wa kufanya kazi ili kufikia muda uliowekwa na TAMISEMI, aliongeza pia ni lazima wazingatie vipimo vilivyotolewa sanjari na kutumia busara ili kutopoteza uhalisia wa ramani iliyochorwa.
Katika ziara yake ambayo aliambatana na wataalamu mbalimbali kutoka mkoani ambapo Injinia Siro Mrioka alisema kuwa ni vizuri kazi inavyofanyika huku akitoa baadhi ya maelekezo na kushauri mafundi kufanya kazi kwa kutumia mpango kazi.
Juu ya swala hilo Katibu Tawala alielekeza kuwa Wilaya inaweza kutumia majeshi kama njia mbadala ili kuongeza nguvu kazi ambapo alitaja jeshi la magereza kuwa linaweza kusaidia katika kazi hiyo huku akizidi kusisitiza juu ya ushirikiano kati watu wa manunuzi na injinia wa mradi ili kubaini vifaa vinavyohitajika na kuvifanyia kazi upatikanaji wake.
Sanjari na hayo Injinia wa TARURA, Filbert Mpalasinge alisema kuwa wamefanya marekebisho kwenye jengo la mionzi kulingana na maelekezo yalivyotoka TAMISEMI ambapo yaliwataka kujenga kuta zenye ukubwa utakaoweza kuzuia mionzi kutopenya na kuwaathiri watu wengine.
RAS pamoja na msafara wake wakipata maelezo toka kwa injinia Mpalasinge juu ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
Akipokea maelekezo Mkurugenzi Mtendaji (W) Bi. Martha Luleka alisema kuwa Halmashauri ya Sikonge imefaanya kazi kwa ushirikiano huku akitaja kuwa miongoni mwa mambo wanayoyatekeleza ni kutumia mapato ya ndani katika kupata maji yanayotumika kuendeshea shuguli za ujenzi.
Pia aliwapongeza wadau mbali mbali waliojitokeza kusaidia mradi huo, huku akiomba kufikiriwa kwa swala la maji, na umeme ambao haupo katika pesa iliyotolewa hivyo inailazimu Halmashauri kufanya kazi ya ziada kuhakikisha pesa hizo zinapatikana.
Naye Mkuu wa Wilaya Mhe. Peres Magiri alitoa shukrani zake kwa ugeni huo na kuahidi kuyatekeleza yale yote yaliyoelekezwa kwa kuhakikisha kazi zinafanyika kwa ubora na kukabidhi kazi kwa wakati.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA TEKINOLOJIA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA)
SIKONGE.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa