Na. Robert Magaka – Sikonge.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Kupitia Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi imewezesha upatikanaji miche bora mia tano ya mti wa mwembe kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo SUA ili kuboresha afya shuleni.
Miti hiyo imesambazwa katika kata ya Sikonge na Misheni ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian kama lilivyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha katika Vikao vya kawaida vya Lishe Wilayani Sikonge.
Aidha Mkuu wa Divisheni ya Kilimo.Mifugo na Uvuvi Bw. Hashim Kazoka amesema zoezi hili ni endelevu miche hiyo itaendelea kusambazwa katika kata zote za Wilaya ya Sikonge ikiwa ni pamoja na kuwagawia wananchi kwa utaratibu utakaopangwa.
#Sikonge tunazingatia utekelezaji wa Afua za Lishe kwa Vitendo.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa