"NITAENDELEA KUOMBA FEDHA SERIKALINI KWA AJILI YA MAENDELEO YA SIKONGE" MHE.KAKUNDA
Mbunge Jimbo la Sikonge Mhe.Joseph Kakunda amekutana na kuzungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kisanga akisema Serikali ya awamu ya Sita inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma mbalimbali kwa wananchi akitoa mfano Tsh.milioni 500 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya kusambaza maji kwa wananchi wa Kata ya Kisanga na vijiji vyake huku akiongeza kuwa huduma za umeme zinaendelea kuboreshwa.
Aidha,ameongeza kuwa ataendelea kuisemea Wilaya ya Sikonge kwa Serikali ili iendelee kutengewa fedha za miradi ya maendeleo ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Kwa upande wake Diwani Kata ya Kisanga Mhe.Yusuph Ahmed amempongeza Mbunge kwa kuendelea kutatua changamoto za maendeleo katika kata hiyo, huku akiipongeza Serikali kwa juhudi kubwa inazofanya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii.
Miongoni mwa kero walizowasilisha ni pamoja na Upungufu wa maeneo ya malisho kwa wafugaji suala ambalo ameahidi kulifanyia kazi.
Na.Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa